Hebrews 1:10-12

10 aPia asema,

“Hapo mwanzo, Ee Bwana, uliweka misingi ya dunia,
nazo mbingu ni kazi ya mikono yako.
11 bHizo zitatoweka, lakini wewe utadumu;
zote zitachakaa kama vazi.
12 cUtazikungʼutakungʼuta kama joho,
nazo zitachakaa kama vazi.
Lakini wewe hubadiliki,
nayo miaka yako haikomi kamwe.”
Copyright information for SwhNEN